12.09.2015


Chadema ‘wapotezea’ ahadi ya kuuza gari la Meya

imeandikwa
                na 
                            James ze navigator

MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameipotezea ahadi ya kuuza gari la kisasa lililokuwa likitumiwa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi (CCM) waliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Wakati wa kampeni hizo, madiwani hao pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa walisema wataliuza gari hilo la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser Prado ili fedha zitakazopatikana zitumike kununua gari la kubeba wagonjwa kwa ajili ya hospitali ya manispaa hiyo.
Hospitali hiyo inayotoa huduma wakati ujenzi wake ukiendelea imejengwa ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
Katika kampeni hizo, wagombea hao wa Chadema waliwalaumu waliokuwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo 2010-2015 ambao kwa asilimia 99 walichaguliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupitisha uamuzi waliouita wa kipuuzi wa kununua gari hilo huku hospitali hiyo ikiwa haina gari la kubeba wagonjwa.
Katika mikutano yao mbalimbali ya kampeni, Chadema waliwaomba wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini wamchague mgombea wao ubunge na wagombea wake ili wakafanye maamuzi mengi yenye maslahi mapana kwa wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuuza gari hilo ili fedha zake zikanunue gari la kubeba wagonjwa.
Ahadi hiyo na nyingine nyingi za chama hicho zilipokelewa na wapiga kura wa mjini Iringa kwa kumchagua kwa awamu nyingine ya miaka mitano Mchungaji Msigwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na kuwachagua madiwani 14 kati ya 18 wa jimbo hilo, kuunda halmashauri ya manispaa hiyo.
Wakizungumza na wanahabari hivi karibuni, Meya wa Manispaa hiyo, Alex Kimbe na Naibu wake Joseph Lyata walisema mpango wa kuuza gari hilo haupo tena kwa sababu taratibu za kupata gari la wagonjwa zinaendelea kufanywa kwa kasi kubwa.
“Ni kweli kulikuwa na ahadi ya kuuza gari hili ili fedha zake zitumike kununua gari la wagonjwa, mpango huo haupo tena kwa sababu kuna mipango mingine ya kupata fedha zitakazotumika kununua gari rasmi la wagonjwa,” alisema Naibu Meya Lyata.
Lyata alisema kwa kuzingatia mpango huo, gari hilo litaendelea kutumika kwa matumizi ya Meya, Naibu wake na kwa shughuli nyingine za halmashauri pale inapolazimu.


Kata ya Ipala Dodoma yapata Diwani wake 


GEORGE Magawa jana alitangazwa kuwa Diwani wa Kata ya Ipala katika wilaya ya Dodoma Mjini baada ya kupita bila kupingwa kutokana na wagombea wawili wa nafasi hiyo kujitoa.
Wagombea waliojitoa ni Shukuru Mahinga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Amani Madelemo wa Chama cha ACT Wazalendo.
Akimtangaza mshindi huyo, Mtendaji wa Kata ya Ipala, Hamisi Jigwa alisema wagombea wengine wamejitoa baada ya kufuata utaratibu.
“Kutokana na hilo ninamtangaza George Magawa kuwa Diwani wa Kata ya Ipala,” alisema Jigwa.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba alisema kata hiyo ilikuwa upinzani kwa vipindi kadhaa na sasa imerudi CCM.
Alisema upande wa wapinzani waliamua kujitoa baada ya kuona kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.
“Kwa kutumia hekima wameona wafanye hivyo kutokana na kuridhishwa na kasi ya utendaji wa Rais,” alisema.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo aliwashukuru wananchi kwa kutoa kura nyingi kwa mgombea wa nafasi ya Urais Dk Magufuli na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde.
Naye Diwani Magawa alisema atafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa.
Uchaguzi katika kata hiyo uliahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema, Victoria Mgabe (55) kufariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki wakati wa akivuka barabara.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 11 mwaka huu katika eneo la Wajenzi mtaa wa Area C.
Uchaguzi mdogo ulikuwa ufanyike Jumapili wiki hii pamoja na kata nyingine za Nyamilolelwa katika Halmashauri ya Geita na Mvomero katika Halmashauri ya Mvomero.
Pia siku hiyo kutafanyika uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Arusha Mjini mkoani Arusha na Handeni mkoani Tang

12.08.2015

Mafuriko yasababisha maafa DR Congo;
Nchini Jahmuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji wa Kinshasa, watu zaidi ya 20 wamefariki na nyumba kadhaa kujaa maji kutokana na mafuriko.makubwa yaliyo tokea leo mchana kutokana na mvua iliyonyesha kwa zaid ya masaa matu

wahitimu chuoni mzumbe wahimizwa ktumia elimu zao vyema
 
WAHITIMU Chuo Kikuu Mzumbe wameshauriwa kutumia elimu waliyoipata katika kuchochea maendeleo ya chuo hicho na ya taifa kwa ujumla. Rais wa Masajili ya chuo hicho, (Mzumbe University Convocation), Ludovick Utouh ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu mstaafu wa Hesabu za Serikali, alitoa mwito huo katika mkutano wa masajili ya 15 ya chuo mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.
“Wote tuliosoma hapa na tukapata muongozo mzuri wa elimu na kufikia nafasi tulizonazo mahali popote tulipo, tujione tuna wajibu wa kushiriki kukisaidia chuo chetu,” alisema Utouh.
Awali, kabla ya kuwa Chuo Kikuu, kilijulikana kama Chuo cha Maendeleo Mzumbe (IDM).
Alisema michango inayohitajika kutoka kwa wahitimu hao ni pamoja na mawazo yao ya kitaaluma katika kuboresha mitaala, kuboresha miundombinu, kubadilishana uzoefu na mawazo.
Akitoa mfano alisema wale wote ambao wamekuwa wakishiriki katika kukisaidia wamefanikisha kujenga Bweni la Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wanawake na kutatua changamoto mbalimbali chuoni hapo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Josephat Itika alisema wamepanga Juni 24 mwakani kufanya mkutano utakaowakutanisha wahitimu wote waweze kutoa michango yao na kubadilishana mawazo na uzoefu kwa maendeleo ya chuo.
Aliwataka wahitimu hao ambao hawajajiorodhesha katika masajili ya chuo kufanya hivyo kupitia tovuti ya chuo ya www.mzumbe.ac.tz ili kurahisisha mawasiliano na wenzao.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Profesa Daniel Mkude alitoa zawadi kwa wahadhiri waliochapisha machapisho mbalimbali na kuwataka kuendelea kufanyakazi hiyo na kuzidi kuboresha maudhui.
“Hii ni taasisi ya elimu ya juu na wahadhiri pamoja na kazi ya kufundisha pia mna wajibu wa kufanya tafiti na kuandika machapisho mbalimbali,” alisema.
Sambamba na hilo pia alitoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao na kuwataka kuongeza bidii katika kutafuta maarifa zaidi nje ya taaluma zao.




JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema limeanza kuchukua hatua kali kwa watu waliohusika na upigaji wa picha wa vifaa vya kijeshi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, ambapo hadi sasa tayari watu wanne wapo chini ya ulinzi.




SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuwa, ifikapo mwezi ujao umeme unaotokana na gesi unaozalishwa nchini utafikia megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Hayo yatakuwa ni mapinduzi makubwa kwani miaka mingi vyanzo vya maji


RAIS John Magufuli ameendelea kutumbua majipu katika maeneo mbalimbali yenye harufu ya ufisadi, ambapo safari hii ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya kupisha uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya kiasi cha Sh bilioni 13 katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).


MKUU wa Mkoa wa Katavi, Dk Ibrahim Msengi amewasimamisha kazi maofisa waandamizi 11 wa Manispaa ya Mpanda akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wake, Suleiman Lukanga kwa ukiukwaji wa sheria za manunuzi kwa kufanya ubadhirifu fedha zaidi ya Sh milioni 92.8.
ndivyo vilikuwa vikichangia kwa asilimia 70.

 

 

AGIZO la Rais John Magufuli la kutaka Sikukuu ya Uhuru itakayoadhimishwa kesho, inakuwa ya kufanya usafi, limeanza kutekelezwa kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali nchini.




Mwezi mmoja wa uongozi wa Magufuli Tanzania

 

7 Disemba 2015 Imebadilishwa mwisho saa 16:18 GMT
Ni siku thelathini tu tangu rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli aingie madarakani, lakini kasi ya utendaji wake umeibua hisia mbalimbali nchini humo, nchi za jirani na hata zingine za mbali barani Afrika.
Kuanzia kuwasimamisha kazi maofisa waandamizi wa serikali na mashirika ya umma hadi kufuta kwa sherehe za maadhimisho kadhaa utendaji wake umetia shauku ya watu kutaka kujua uongozi wake utaleta chachu gani nchini Tanzania.
Mwandishi wa BBC Sammy Awami amedodosa hilo zaidi.
kwa habar zaidi bofya
http://www.bbc.com/swahili/medianuai/2015/12/151207_30_days_magufuli_presidency
ANGALIA KICHEKESHO HIKI CHA WHATSAPP 
NI HATARI SANA INACHEKESHA SANA 

tazama na kuidownload

hapa chini

 
 download/tazama

download ngoma mpya nash mc

Yabaki ,masaa machache ambapo watanzania wote nchini wataungana kusheherekea sherehe yamuungano kwa namna ya tofauti tangu taifa hili lipate uhuru haijawahi tokea ambapo watasherekea kwa kufanya usafi maeneo yanayo wazunguka hii ni kutokana na dokta john pombe magufuli Raisi ya wa muungano wa tanzania alitangaza ili watanzania waweze kujiepusha na mazingira hatarishi yanayoweza sababisha watu kupata kipindupindu hivyo siku ya kesho ambayo ni tarehe 9/12 watanzania wataungana na wengine nchii nzima kufanya usafi ..............

mabwana afya na bibi afya  watakua wakizunguka mtaani kwani wao ndo wahusika wakuu kuhakikisha usafi ukiendelea na kwa kiwango kinxhotazamiwa

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...