12.09.2015

Kata ya Ipala Dodoma yapata Diwani wake 


GEORGE Magawa jana alitangazwa kuwa Diwani wa Kata ya Ipala katika wilaya ya Dodoma Mjini baada ya kupita bila kupingwa kutokana na wagombea wawili wa nafasi hiyo kujitoa.
Wagombea waliojitoa ni Shukuru Mahinga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Amani Madelemo wa Chama cha ACT Wazalendo.
Akimtangaza mshindi huyo, Mtendaji wa Kata ya Ipala, Hamisi Jigwa alisema wagombea wengine wamejitoa baada ya kufuata utaratibu.
“Kutokana na hilo ninamtangaza George Magawa kuwa Diwani wa Kata ya Ipala,” alisema Jigwa.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba alisema kata hiyo ilikuwa upinzani kwa vipindi kadhaa na sasa imerudi CCM.
Alisema upande wa wapinzani waliamua kujitoa baada ya kuona kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.
“Kwa kutumia hekima wameona wafanye hivyo kutokana na kuridhishwa na kasi ya utendaji wa Rais,” alisema.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo aliwashukuru wananchi kwa kutoa kura nyingi kwa mgombea wa nafasi ya Urais Dk Magufuli na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde.
Naye Diwani Magawa alisema atafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa.
Uchaguzi katika kata hiyo uliahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema, Victoria Mgabe (55) kufariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki wakati wa akivuka barabara.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 11 mwaka huu katika eneo la Wajenzi mtaa wa Area C.
Uchaguzi mdogo ulikuwa ufanyike Jumapili wiki hii pamoja na kata nyingine za Nyamilolelwa katika Halmashauri ya Geita na Mvomero katika Halmashauri ya Mvomero.
Pia siku hiyo kutafanyika uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Arusha Mjini mkoani Arusha na Handeni mkoani Tang

No comments:

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...