1.01.2016

Ngumi za mabonge



James ze navigator

‘Dar ina maeneo ya wazi 180 yaliyovamiwa’


JIJI la Dar es Salaam lina maeneo ya wazi 180 ambayo yamevamiwa, ambapo 111 yapo Halmashauri ya Kinondoni, 50 yapo Ilala na Temeke yapo 19. Hayo yamebainishwa wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, walipozungumza na waan
Makamba alifafanua kuwa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 imeweka makatazo mahsusi kwa nia ya kuepusha uharibifu wa mazingira, ambapo Kifungu cha 57 cha sheria hiyo, kinazuia shughuli zozote zinazoweza kuhatarisha au kuathiri mazingira kutofanyika ndani ya mita 60 katika kingo za mito, maziwa na bahari ili kulinda maeneo hayo.
“Tunawaomba wale wote waliokiuka sheria hii, wabomoe wenyewe, vinginevyo tutaanza kubomoa wenyewe na hatutamuonea huruma mtu,kwa sababu mazingira yameharibiwa sana”, alisema Makamba.
Alisisitiza kwamba wale wote waliojenga kwenye fukwe, na kingo za maziwa na bahari, waanze kuondoka wenyewe, kwa sababu wizara inaanza kutekeleza sheria ya mazingira kikamilifu.
“Tukimaliza kubomoa maeneo ya ufukweni na kwenye kingo za mito na maziwa nchi mzima , tutahamia kwenye maeneo ya wazi, watu waondoke wenyewe wasingoje kubomolewa,” alisisitiza Makamba.
Kwa upande wake, Lukuvi alisema kuanzia Januari mwakani ataongoza kazi ya kugawa vipisi vya ramani za maeneo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa nchini, zinazoonesha matumizi ya ardhi kwa eneo husika.
Alisema eneo la bonde la mto Msimbazi, linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,927 mara baada ya bomoabomoa kumalizika, eneo hilo linaandaliwa kwa ajili ya kutengenezwa maeneo ya burudani kwa umma.
Alisema eneo hilo ni kuanzia daraja la Selander hadi Vingunguti pamoja na maeneo mengine ya bonde hilo. Lukuvi alisema serikali imesimamisha kazi ya bomoabomoa kwa siku 15, kwa wavamizi waliojenga katika Bonde la Mto Msimbazi na kuwataka wavamizi hao kubomoa wenyewe na kuondoka maeneo hayo kabla ya kazi hiyo kuanza tena Januari 5 mwakani.
r

Niyonzima asema hana furaha 

James ze navigator

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema hana furaha kuwa nje ya Yanga na kuwataka mashabiki kuwa wavumilivu kwani suala lake linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuwasilisha maelezo yake kwa uongo
Akizungumza na gazeti hili jana Niyonzima alisema Yanga ni timu yake na ameishi nayo vizuri pamoja na watu wake hivyo anaamini tofauti zao zitamazilika na kurejea kuitumikia.
“Yanga ni timu yangu na nimeishi nayo vizuri pamoja na watu wake, lakini sina furaha kwani nimekaa nje kwa muda usiojulikana lakini haya yote ni majaribu na najua ni vitu ambavyo vipo duniani ila naamini yataisha vizuri tu,” alisema.
“Mimi ni binadamu naweza kufanya makosa lakini nawahakikishia wapenzi wa Yanga na wa Niyonzima kwamba hili litaisha siku si nyingi na wataendelea kupata burudani kama ilivyokuwa na zaidi”.
Pia aliwatakia heri Yanga kwenye mchezo wa leo na heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2016 na kuwataka wamalize mwaka 2015 kwa amani. Niyonzima amesimamishwa kwa muda usiojulikana na uongozi wa Yanga kutokana na kuchelewa kurudi kujiunga na timu hiyo baada ya kumalizika kwa mashindano ya Chalenji iliyofanyika Ethiopia ambapo yeye alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda

SHERIA YA KUZUIA KELELE YAANZA KUNG'ATA

James ze navigator


Sheria kuzuia kelele yaanza kung’ata 


BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo. Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10.
Pia, baa na kumbi za starehe za usiku zitakazopiga kelele, zitapaswa kulipa kiasi hicho. Aidha, NEMC imesema pia kuwa wale watakaohusika na kelele za migodini za kutumia baruti, kupasua miamba zilizo zaidi ya matakwa ya sheria ya mazingira ya kelele na mitetemo, watapaswa kulipa Sh milioni tano ili kupata kibali.
NEMC imetaka watu kuheshimu kanuni za viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali nchini. Imeonya kuwa watakaokiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kanuni hizo zimeanza kutumika mwaka jana (2015).
Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Bonaventure Baya alisema hayo Dar es Salaam jana. Alisisitiza kuwa uchafuzi wa mazingira, unaosababishwa na kelele na mitetemo, umekuwa ukifanyika bila kujali sheria za nchi na sasa watashughulikia suala hilo ipasavyo.
Alisema hivi sasa kanuni za kudhibiti suala hilo, zimekamilika na zimeanza kutumika kikamilifu. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha kanuni na sheria, atachukuliwa hatua kali. Baya alitoa ufafanuzi kuwa yapo maeneo yenye kelele zaidi ya viwango vinavyoruhusiwa kisheria, ikiwamo maeneo ya migodini.
Alieleza kwamba kanuni zimeweka vigezo na tozo maalumu la kuanzia Sh milioni tano hadi Sh milioni 10, kulingana na eneo na aina ya kelele na mtetemo. Alisema mambo mengine ambayo kanuni zimeweka ni faini kwa kila kanuni itakayovunjwa na kusisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa ipasavyo.
Kulingana na hatua hiyo ya NEMC, sasa mtu mwenye kutaka kufanya sherehe mtaani, itakayohuisha kelele zitakazosumbua jamii pamoja na majirani zake, ikiwamo muziki maarufu wa ‘kigodoro’, ibada za makanisani zinazozidi matakwa ya kisheria ya uanzishwaji wa makanisa hayo katika jamii, atapaswa kulipa Sh milioni 10 ndipo aruhusiwe kuendelea na shughuli yake.
Kwa mujibu wa NEMC, ruhusa hiyo inayo lipiwa, pia ina muda na viwango vyake, ambapo kila muda husika unapoisha, kelele zinapaswa kupunguzwa ama kuzimwa. Hii inahusisha pia baa na kumbi za starehe za usiku.
Baya aliitaka jamii kuepuka uchafuzi huo wa mazingira wa kelele na mitetemo, ambao watu wengi wamekuwa wakidhani si tatizo. Alitaka watu kuheshimu matakwa ya sheria na kanuni kwa nyakati za mchana na usiku.
“Tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watu wengi, wakilalamikia usumbufu wa kelele na mitetemo kutoka kwa watu wanaoendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika jamii,” alifafanua Baya.
Alitoa angalizo kwa wanaotumia vyombo vya muziki na sauti katika maeneo ya makazi, ambavyo vimeleta madhara kwa afya za watu. Alisema matumizi ya vipaza sauti na vyombo vya sauti kubwa, wanapaswa kuwa na kibali maalumu.
Alieleza kuwa kanuni za kelele na mitetemo, zimeweka vigezo na viwango vya sauti kwa ajili ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya hospitali, makazi, migodini, kumbi za kijamii, kumbi za usiku za starehe, matangazo, baa na maeneo mengine.
Baya alisema baraza limepata changamoto kadhaa, ikiwamo uelewa mdogo wa jamii kuhusu kiwango cha sauti kinachotakiwa na kisichoruhusiwa na baadhi ya watu kwa makusudi huvunja sheria.
Kuhusu faini, alisema sheria ya mazingira imeweka wazi faini kwa wanaokiuka na kuchafua mazingira kwa kelele na mitetemo. Faini hiyo haiingiliani na tozo la Sh milioni tano hadi Sh milioni 10 lililoelezwa, ambapo mtu anapaswa kulipa si chini ya Sh milioni 50 na si zaidi ya Sh milioni 50 ama kifungo jela.
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sheria za Mazingira wa NEMC, Ruth Lugwisha alisema tatizo la kelele na mitetemo, limekuwapo kwa muda mrefu. Alisema tangu kupitishwa kwa kanuni, tayari watu kadhaa wamewajibishwa.
Alisema miongoni mwa waliowajibishwa ni makanisa, kumbi za starehe na baa. Hata hivyo, hakuwa tayari kuwataja wahusika wala maeneo. Alisema uwajibishwaji huo ulihusisha faini, kufungiwa na onyo.
Tukio la Masasi Oktoba mwaka huu wakazi wanne wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, walifikishwa mahakamani kwa kosa la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya ‘vigodoro’ kwenye sherehe ya ndoa.
Wakazi hao ni Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa). Watuhumiwa hao baada ya kupatikana na hatia, walilipa faini na kuachiwa huru.
Maoni ya wananchi wa Tanga Huko Tanga, baadhi ya wananchi walisema hivi karibuni kuwa matamasha na promosheni mitaani, sasa zimekuwa kero. Waliomba idara ya utamaduni kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazohusika na utoaji wa vibali kwa ajili ya mikutano, maonesho na matamasha jijini Tanga, kupunguza kero ndani ya jamii.
Walitaka mamlaka hizo, kuacha kutoa vibali vya matamasha ya burudani na starehe zisizo na staha katika jamii, kwa sababu zinasababisha kelele mitaani na kuwanyima wanafunzi muda wa kujisomea.
Wananchi hao walidai matamasha yanayoambatana na kelele za ngoma na muziki, yanakwamisha ustawi wa elimu na kukua kwa kiwango cha taaluma, hasa kwa wanafunzi wa sekondari.
Damas Mboya, mkazi wa Ngamiani, alisema matamasha na promosheni zinazofanyika mitaani nyakati za mchana na usiku, hudumaza maadili na ni kero kwa jamii kwakuwa zinatumia vipaza sauti kucha usiku kucha.
Merina Kimweri, mkazi wa Chumbageni, alisema “Naishauri serikali na mamlaka husika, zipunguze idadi ya vibali vya kuruhusu shughuli hizi, hasa zinazofanywa mitaani bila viingilio.
Nasema hivyo kwa kuwa mara kadhaa zinaambatana na burudani za ngoma za kukesha, maarufu kama vigodoro na baikoko ya usiku, ambapo washiriki wakuu ni wanafunzi”

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...