12.08.2015




JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema limeanza kuchukua hatua kali kwa watu waliohusika na upigaji wa picha wa vifaa vya kijeshi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, ambapo hadi sasa tayari watu wanne wapo chini ya ulinzi.




SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuwa, ifikapo mwezi ujao umeme unaotokana na gesi unaozalishwa nchini utafikia megawati 700 sawa na asilimia 70 ya umeme wote kwenye Gridi ya Taifa. Hayo yatakuwa ni mapinduzi makubwa kwani miaka mingi vyanzo vya maji


RAIS John Magufuli ameendelea kutumbua majipu katika maeneo mbalimbali yenye harufu ya ufisadi, ambapo safari hii ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya kupisha uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya kiasi cha Sh bilioni 13 katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).


MKUU wa Mkoa wa Katavi, Dk Ibrahim Msengi amewasimamisha kazi maofisa waandamizi 11 wa Manispaa ya Mpanda akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wake, Suleiman Lukanga kwa ukiukwaji wa sheria za manunuzi kwa kufanya ubadhirifu fedha zaidi ya Sh milioni 92.8.
ndivyo vilikuwa vikichangia kwa asilimia 70.

 

 

AGIZO la Rais John Magufuli la kutaka Sikukuu ya Uhuru itakayoadhimishwa kesho, inakuwa ya kufanya usafi, limeanza kutekelezwa kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali nchini.




No comments:

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...