6.30.2017
Halmashauri zinazotaka nyumba NHC zashauriwa kujiandaa
Halmashauri zinazotaka nyumba NHC zashauriwa kujiandaa
HALMASHAURI zinazotaka kujengewa makazi na Shirika la Nyumba Taifa (NHC) zinatakiwa kutenga maeneo, kulipa fidia na kuweka miundombinu.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanislaus Nyongo (CCM). Nyongoa alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kulialika NHC kujenga nyumba katika mkoa mzima wa Simiyu.
Mabula alisema hadi sasa halmashauri mbili za Busega na Bariadi ndizo zimetenga maeneo kwa ajili ya NHC kujenga nyumba, na zinazobaki zinatakiwa kutenga maeneo, kuwalipa fidia wananchi wenye maeneo na kuweka miundombinu ili kujenga nyumba hizo. Alisema halmashauri hizo zinatakiwa kuwa na uhakika wa matumizi ya nyumba hizo, kwani kuna halmashauri 30 ambazo zimejengwa nyumba na NHC na hazitumiki.
Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga (CCM) aliyetaka kujua ni lini ahadi ya Rais ya wakati wa Kampeni mwaka 2015 itatekelezwa ya kujenga za watumishi katika wilaya ya Itilima, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alisema katika mwaka 2017/18, serikali imetenga Sh milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za watumishi.
“Katika mwaka wa fedha 2016/17, serikali ilitenga Sh milioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za watumishi,” alisema. Aidha, serikali imetoa Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na ujenzi wake unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Serikali yatoa siku saba walimu kupewa posho
Serikali yatoa siku saba walimu kupewa posho
SERIKALI imetoa siku saba kwa ajili ya halmashauri zote kuhakikisha walimu wa hesabu, sayansi na wataalamu wa maabara waliopangwa hivi karibuni wanapewa posho za kujikimu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema). Mkundi alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu, Sayansi na watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni. Alisema halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za kujikimu ndani ya siku saba.
Akijibu swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya pembezoni, alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya ikiwemo halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa motosha kwa watumishi.”
Alisema kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya motisha inayohitajika. “Utekelezaji wa miongozo hiyo kwa halmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh bilioni 331.087 kwa mwaka na utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu wa bajeti
Subscribe to:
Comments (Atom)
MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO
UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018 MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...
-
james ze navigator the blogger boy karibuni iringa mjini angalia picha za mij wa iringa kwa kutumia picha zenye ubora wa hali ya...
-
Special need education is defined as a particular educational requirements resulting from learning difficulties such as physical disabilit...