Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Afanya Ziara Katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi jijini Dar.......Aagiza Yaanze Kufanya Kazi Ifikapo Januari 10 Mwakani
James ze navigator
Mradi wa
Mabasi yaendayo haraka (BRT) utaanza Januari 10, 2016.Hayo yamesemwa na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akikagua ujenzi wa miundo
mbinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.
Pia
Majaliwa amewaagiza watendaji wizara ya Tamisemi ambao ni wamiliki wa
mradi huo kusimamia vyema ili uanze kufanya kazi kama ilivyo pangwa
kwa kuwa mabasi 120 yalishawasili jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ameanza kwa kukagua vituo vya mradi huo kuanzia cha
Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa
kumaliza kujenga vituo 15 kati ya 27 na amewaagiza kumalizia vituo
vilivyo baki ili kufikia januari 10 mwakani mabasi yaanze kufanya kazi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na watendaqji
mbalimbali wa mradi wa mabasi yaendayo haraka waliofika katika kituo cha
Feri cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es
Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda basi la mwendo wa
haraka mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali katika kituo cha feri
leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika kituo cha Mradi
wa mabasi cha Jangwani kukagua maendeleo ya ujenzi ya kituo hicho ikiwa
ujenzi wa kituo hicho upo hatua za mwisho kukamilika
by james ze navigator

No comments:
Post a Comment