James ze navigator
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema unaunga mkono kasi ya utekelezaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli na kwamba anachofanyika sasa ndio kiu ya Watanzania.
Aidha umoja huo umesema utaendelea kumuunga mkono kila hatua kwa lengo la kuona vijana wote wa Tanzania wanarudi katika ari ya uwajibikaji kama ilivyokuwa wakati wa serikali ya awamu ya kwanza.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuongoza ufanyaji usafi katika eneo la Soko la Kigogo, Dar es Salaam.
“Kinachofanywa sasa na serikali ya CCM ya awamu ya tano ni matokeo ya ubora wa sera zilizomo kwenye ilani yake ya uchaguzi, tumeahidi, tumedhamiria na sasa tunatimiza ahadi za Chama,” alisema Shaka.
Shaka alikuwa akijibu swali aliloulizwa kama yanayotekelezwa sasa na serikali ya awamu ya tano, yanatokana na ilani ya uchaguzi ya CCM. Kwa mujibu wa Shaka, UVCCM itaendelea kumuunga mkono kwa vitendo Dk Magufuli katika dhamira na malengo ya serikali yake, hasa kupiga vita rushwa, maonevu, ubadhirifu wa mali za umma, mkakati wa udhibiti na matumizi bora ya rasilimali na maliasili za Taifa pamoja na kuhimiza uwajibikaji maeneo ya uzalishaji mali.
“Tutamuunga mkono kwa hali na mali, tutawakabili na ikibidi kuwaumbua watakaothubutu kumsakama au kumkwamisha, tunahitaji kasi ya kuwatumikia wananchi ili nchi ipige hatua zaidi kiuchumi, “alisema.
Kuhusu kasi yake serikali yake katika kuwachukulia hatua watendaji wazembe, kuwaweka kando wale tuhuma za ufujaji na wizi wa fedha za serikali, Shaka amesema wakati wa kubebana umekwisha na sasa ni kazi kwenda mbele.
“Ulikuwa ni mwezi mmoja wenye maajabu, matumaini na mararajio katika utendaji wa Serikali inayotumikia wananchi wake, tunataka Dk Magufuli zaidi kutumbua zaidi majipu na kusafisha uchafu, “alisisitiza Shaka.
UVCCM yampa tano Rais Magufuli

No comments:
Post a Comment