12.20.2015

James ze navigator
Majaliwa ataka mabasi ya kasi yawe barabarani
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, ameagiza Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuhakikisha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), unaanza kufanya kazi Januari 10, mwakani. Kadhalika, ameagiza wizara hiyo kupitia upya mikataba ya wadau wa mradi huo, wakiwemo Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine kwenye mradi huo, ili kurekebisha kasoro zilizopo kwa lengo la kuhakikisha Serikali inanufaika.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo Dar es Salaam jana, wakati akikagua vituo vya mradi huo kuanzia eneo la Kivukoni hadi Kimara na kisha kituo cha Morocco, Kinondoni. Alisema kati ya vituo vya kupakia na kushukia abiria 27 vya mradi huo, vituo 15 viko kwenye hatua za mwisho za kukamilika, hivyo kuitaka wizara hiyo kuhakikisha Januari 10, mwakani, mradi huo unaanza kazi kwa vituo vilivyokamilika.

“Vituo vikuu vitano lazima vianze kazi Januari 10, mwakani na kasoro zilizopo zifanyieni marekebisho, ikiwemo kubadilisha vigae kwenye baadhi ya vituo kama kile cha Kivukoni, kazi hiyo ifanyike kwa wakati na nitarudi tena mwisho wa mwezi huu, kukagua kabla mradi haujaanza kazi,” alisema Majaliwa.

Alivitaja vituo vikuu vitano vitakavyotakiwa kuanza kazi Januari 10 kuwa ni Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni.

Akizungumzia kasoro za vigae kwenye kituo cha Kivukoni, Waziri Mkuu Majaliwa alisema vigae vilivyotumika si sahihi na viko chini ya kiwango na kumtaka mkandarasi kuanza kuvivunja na kuweka vingine vyenye ubora, vitakavyokuwa rafiki kwa wasafiri.

Kuhusu kupitia upya mikataba ya wadau wa mradi huo, Waziri Majaliwa alimwagiza Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene, kupitia upya mikataba iliyoingiwa baina ya wadau hao na kuhakikisha kasoro zilizopo zinafanyiwa kazi kabla ya mradi kuanza, ili Serikali inufaike na mradi huo.

Alisema pamoja na kufanyiwa marekebisho hayo, pia Wizara inapaswa kuthamini wadau wa daladala, ambao mara baada ya kuanza kwa mradi huo, magari yao yatakosa kazi, hivyo waangalie jinsi ya kuwaingiza kwenye mradi kwa wale wenye sifa.

“Mradi huu utakapoanza, ina maana daladala zitaondoka barabarani, sasa Wizara ithamini wadau hao na wenye sifa muwaingize kwenye mradi ili kuondoa malalamiko yasiyo na msingi,” alisema Majaliwa. Aliongeza kuwa, Serikali kama mwendeshaji wa mradi huo, imetoa fursa kwa wawekezaji kutoa huduma za usafiri na kwamba ni vyema mfumo wa tiketi ambao umeshafungwa na mwekezaji, uchunguzwe na Serikali ili kudhibiti mapato.

Alisema kabla ya mradi huo kuanza kazi, Wizara na mamlaka husika zitatakiwa kuingia mikataba na wawekezaji wa mradi huo, ili kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake na watakaoshindwa wawajibike.

Majiko ya feri Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Ilala, kubadilisha mfumo wa majiko yanayotumika kukaangia samaki eneo la Feri na kuweka ya kisasa yatakayodhibiti moshi.

Alisema hivi sasa hali si shwari eneo la Feri kutokana na eneo lote kuzingirwa na moshi, ambao licha ya kuathiri wafanyabiashara sokoni hapo, lakini pia unaharibu mazingira na miundombinu jirani. “Huu moshi udhibitiwe, maana hata hapa mmesikia ninakuja, mkapiga deki, vinginevyo moshi ulikuwa umejaa. Sasa huu ni uharibifu kwa miundombinu, wekeni majiko mapya ya kisasa yasiyotoa moshi, hatuwezi kuendelea kwa moshi huu,” alisema Majaliwa.

Akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Crispinus Ako, Waziri Mkuu alimtaka kusimamia maelekezo yote aliyotoa na kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati.

Agizo lingine la Waziri Mkuu katika kituo cha Kivukoni ni kwa Mkurugenzi huyo pamoja na viongozi wengine, kusimamia ujenzi wa uzio kwenye eneo hilo, ili kudhibiti matukio ya wizi ndani ya kituo hicho. Alisisitiza uwepo wa utaratibu wa kuingia na kutoka kwa mabasi yaletayo na kupakia abiria wanaoshuka kwenye mabasi yaendayo kasi, ili kue

No comments:

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...