12.20.2015

CDA wabomoa nyumba 140 Dodoma

ZAIDI ya nyumba 140 mjini Dodoma zimebomolewa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutokana na wananchi kujenga kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa huku Jeshi la Polisi likilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakileta fujo ikiwemo kufunga barabara kuu ya Dodoma – Singida.
Bomoabomoa hiyo imefanyika katika maeneo ya Chinangali, Ndachi, Barabara ya Bahi na Kizota Dampo katika eneo la Kizota licha ya kutolewa notisi ya siku saba kwa wananchi hao kuondoka, lakini walikaidi amri hiyo ndipo Jeshi la Polisi pamoja na watendaji wa CDA walianza kazi hiyo.
Hata hivyo, wananchi ambao hawakukubaliana na kazi hiyo, walianza kuwarushia polisi mawe.
Baadhi ya wakazi waliangua vilio wengine wakipoteza fahamu baada ya kushuhudia nyumba zao zikibomolewa.
Wakizungumza nje ya nyumba zao, baadhi ya wananchi walisema kazi hiyo ni ya ghafla na hawakupewa taarifa na hawaelewi hatma ya maisha yao kwani hawana pa kulala.
Mkazi wa Kizota Dampo, Mwajuma Khamis alisema alikuwa akitegemea nyumba hiyo kwa ajili ya makazi na sasa hana pa kwenda kufuatia bomoabomoa hiyo.
Mkazi mwingine wa Kizota Dampo, Evania Joseph alisema hawakupewa taarifa yoyote juu ya ubomoaji huo na umefanyika ghafla na kuwaweka katika wakati mgumu.
Kwa upande wake, Ofisa Habari na Mahusiano wa CDA, Angela Msimbila alisema kazi hiyo ni endelevu ambapo wananchi hao walipewa notisi ya siku saba, lakini wamekaidi amri hiyo.
Alisema wananchi walijenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa hali iliyofanya mamlaka hiyo kutekeleza kazi ya ubomoaji.
Wakati kazi hiyo ikiendelea kufanyika katika maeneo mengine, baadhi ya wananchi waliamua kuchukua sheria mkononi na kufunga barabara kuu ya Dodoma-Singida ndipo Polisi ikalazimika tena kwenda na kuwatawanya wananchi hao waliofunga barabara huku mabomu ya

No comments:

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI KIDATO CHA TANO

UPDATES:HIZI HAPA JOINING INSTRUCTIONS ZOTE ZA FORM V/KIDATO CHA TANO(5) 2017/2018   MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SEKONDARI...